IQNA

Ongezeko la Asilimia 10 la Mauzo Nje ya Bidhaa Halali nchini Malaysia

15:52 - August 27, 2018
Habari ID: 3471649
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Ustawi wa Kiislamu Malaysia (Jakim) imetangaza kuwepo ongezeko la asilimia 10 la bidhaa halali zinazouzwa kimataifa kutoka nchi hiyo.

Mkuu wa kitengo cha Bidhaa Halali katika Idara ya Ustawi wa Kiislamu Malaysia Dkt. Sirajuddin Suhaimee anasema kumekuwepo na ongezko kubwa la ununuzi wa bidhaa halali si tu kutoka nchi za Kiislamu bali hata kutoka nchi zisizo za Kiislamu ambazo zinataka bidhaa na huduma halali.

Amesema kati ya nchi zisizo za Kiislamu ambazo zinataka bidhaa zenye  cheti cha Jakim ni pamoja na China, Japan, Taiwan na Hong Kong. Sirajuddin anasema mashirika ya kimataifa ambayo yanataka cheti cha 'Halal' cha Jakim huchukua miezi mitatu kupata cheti hicho. Aidha amesema hivi sasa nchi 42 duniani zimeafiki cheti cha 'Halal' cha Jakim ambapo za hivi karibuni kabisa zilikuwa ni Lithuania na Kazakhstan.

3466622

captcha