IQNA

Misri yawaenzi waliohifadhi Qur'ani

20:55 - October 14, 2018
Habari ID: 3471707
TEHRAN (IQNA)- Zaidi ya washichana na wavulana 500 waliohifadhi Qur'ani Tukufu nchini Misri wamenziwa na kutunukiwa zawadi katika Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani cha Al Minya.

Kwa mujibu wa taarifa, walioenziwa walikuwa wanafunzi walifanikiwa kuhifadhi Qur'ani katika Shule ya Rusulan jimboni la Minya.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya viongozi wa ngazi za juu wakiwemo wajumbe wa Bunge la Misri.
Waalimu wa Qur'ani pia walienziwa katika sherehe hiyo. Shule ya Qur'ani ya Rusulan ilianza shughuli zake na wanafunzi watano mwaka 2001 na imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wanaotaka kuhifadhi Qur'ani.

3755511

captcha