IQNA

Mashindano ya Qur'ani kwa waliosilimu kufanyika Dubai

11:55 - October 27, 2018
Habari ID: 3471720
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa wale waliosilimu yatafanyika mjini Dubai nchini UAE.

Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani na Hadithi za Bwana Mtume SAWyameandaliwa na Kituo cha Maelezo ya Kiislamu (IIC) cha Dubai na Jumuiya ya Dar al Ber ambapo washiriki walikuwa ni wale waliosilimu na watoto wao.
Mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo yanalenga kuwapa fursa ya kuhifadhi Qur'ani walioukumbatia Uislamu maishani hivi karibuni sambamba na kuwapa motisha katika imani.
Mashindano hayo yatajumuisha wanawake na wanaume na mwaka huu kumeanzishwa vitengo vya kuhifadhi Hadithi na pia kitengo cha watoto watakaoshiriki.
Watakaoshika nafasi za kwanza watapata fursa ya kutekeleza Ibada ya Umrah huku waliosaliwa wakitunukiwa fedha taslimu.
Mwaka wa kwanza mashindano hayoyalikuwa na washiriki 100 na idadi hiyo ikaongezeka maradufu mwaka uliofuata ambapo kulikuwa na washiriki kutoka mataifa 28.
Mchakato wa kuwasajili washiriki unamalizika Oktoba 31 na tayari mamia ya wanawake, wanaume na watoto wameshajisajili. Baada ya hapo washiriki watapata mafunzo maalumu ya kujiimarisha kuanzia Novemba 10 na mashindano yatafanyika hatua kwa hatua hadi fainali mnamo Januari 18 katika makao makuu ya Jumuiya ya Dar al Ber katika Barbara ya Sheikh Zayed. Washindi watatangazwa Januari 22 , 2019. Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea tovuti ya www.islamicic.com/quran.

3467076

captcha