Kwa mujibu wa tovuti ya al-Diyar, katika sherehe hizo za Jumanne, wanafunzi 26 waliohifadhi Qur'ani wametunukiwa zawadi. Sherehe hizo zimefanyika katika kijiji cha Atta nje kidogo ya mji wa Idlib.
Wanafunzi hao ambao walikuwa baina ya umri wa miaka 13 hadi 35 waliweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu katika kipindi cha miezi minne.
Harakati za Qur'ani nchini Syria zimeendelea pamoja na kuwa nchi hiyo ilitumbukia katika vita vilivyoibuliwa na magaidi wakufurishaji mwaka 2011.