IQNA

Msichana aliyesilimu Marekani atimuliwa chuoni kwa kuvaa Hijabu

19:41 - December 15, 2018
1
Habari ID: 3471771
TEHRAN (IQNA)- Bi. Linde McAvoy, alisilimu na kuukumbatia Uislamu maishani wiki chache baada ya kujiunga na Chuo cha Georgia Career Institute Conyers (GCI) katika jimbo la Georgia nchini Marekani mwezi Disemba 2017.

Alichagua  taaluma ya vipodozi na alianza kuhudhuria masomo akiwa amevaa vazi la staha la Hijabu na hapo masaibu yake yalianza. McAvoy aliandikia barua chuo cha GCI, kupitia mawakili Waislamu, kulalamikia namna ambavyo anakerwa, kubaguliwa na kubugudhiwa na wakuu wa idara ya chuo hicho kutokana na uamuzi wake wa kuvaa Hijabu.

"Kwa mfano, Joyce Meadows, Mkurugenzi wa GCI,  alianza kusisitiza kuwa Bi. McAvoy avue Hijabu yake, kwa kisingizio kuwa inakiuka taratibu za mavazi darasani," imesema barua ya Mawakili Waislamu. "Hata baada ya Bi.McAvoy kufafanua kuwa anavaa Hijabu kutokana na maamurisho ya Uislamu, Bi. Meadows alisisitiza kuwa lazima avue Hijabu, hii ni pamoja na kuwa taratibu za mavazi hazizuii mitandio ya kidini. Bi. McAvoy amefukuzwa darasani mara kadhaa kutokana na uamuzi wake wa kuvaa Hijabu." Meadows amesisitiza kuwa iwapo McAvoy anataka kuendelea na masomo lazima avue Hijabu wakati akihudhuria darasa.

Nimra Azmi, wakili katika Jumuiya ya Mawakili Waislamu amesema ni muhimu kwa wanawake Waislamu kuvaa Hijabu na kupata elimu. Aidha amesema hakuna ushahidi wowote kuwa kuvaa Hijabu kunakiuka maadili ya kikazi. Mawakili hao wanasema chuo cha GCI kinatekeleza ubaguzi ambao ni kinyume cha sheria na kwamba McAvoy amebaguliwa kwa sababu tu ni Mwislamu anayefungamana na misingi ya dini yake. Sasa McAvoy anataka chuo kimrejeshee karo yake na pia kuwe na sheria maalumu inayoruhusu Hijabu na pia wafanyakazi wa chuo hicho wapate mafundisho yatakayowawezesha kuacha sera zao za ubaguzi.

Kuna ongezeko kubwa la Wamarekani wanaosilimu na wengi wanakumba na matatizo mengi maishani hasa kutengwa katika familia na kubaguliwa katika vyuo vya elimu na sehemu za kazi.

3467465

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Ali khamis
0
0
Allah akbar
captcha