IQNA

Magaidi wa Al Shaba waua watu 16 Mogadishu, Somalia

18:10 - December 22, 2018
Habari ID: 3471781
TEHRAN (IQNA)- Magaidi wakufurishaji wa kundi la Al Shabab wameua watu 16 katika hujuma ya kigaidi iliyojiri leo Jumamosi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Taarifa zinasema gari ambalo lilikue limesheheni mabomu liliripuka katika kituo cha upekuzi wa kijeshi kilichoumbali wa mita 400 kutoka kasri ya Rais wa Somalia. Watu 16 wameuawa huku wengine 20 wakijeruhiwa. Magaidi wakufurishaji wa kundi la Al Shabab amedai kuhusika na hujuma hiyo ya kinyama.

Kati ya walipoteza maisha ni waandishi habari watatu wa televisheni ya Kisomali ya Universal TV yenye makao yake London na miongoni mwao alikuwa mwandishi mashuhuri Awil Dahri.

Maafisa wa usalama wanasema magaidi walilenga kituo hicho cha upekuzi kilicho karibu na mlango mkuu wa kasri ya rais wa Somalia ambayo ina ulinzi mkali.

Kundi la kigaidi la Al Shabab lilianza hujuma zake nchini Somalia mwaka 2007 na limekuwa likiendesha ugaidi katika mji mkuu Mogadishu na maeneo mengine ya Somalia na pia katika nchi jirani ya Kenya. Magaidi hao walitumuliwa Mogadishu Agosti 2011 katika oparesheni iliyofanaya vikosi vya kulinda amani ya Umoja wa Afrika, AMISOM, lakini wamekuwa wakitekeelza mashamabulizi ya kuviziia mara kwa mara.

Kundi la Al Shaba ambalo linafungamana na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda, linafuata itikadi za ukufurishaji Waislamu wasiofuata itikadi za Kiwahhabi na linalenga kuiangusha serikali ya sasa ya Somalia.

3774491

captcha