IQNA

16:35 - December 23, 2018
News ID: 3471784
TEHRAN (IQNA)- Waislamu katika mji wa Liverpool nchini Uingereza wanagawa misaada ya chakula kwa watu ambao hawana chakula katika kipindi cha Krismasi ambacho huandamana na baridi kali mjini humo.

Kwa mujibu wa taarifa, taasisi kadhaa za Kiislamu katika mji wa Liverpool, ambao una msikiti wa kwanza uliowahi kujengwa England, wanakusanya chakula kwa ajili ya kukipelekea katika vituo maalumu amabvyo hugawa chakula kwa watu masikini.

Moja ya vituo vya kukusanya chakula ni chekechea ya Happy Nursery ambapo wasimamisi wanasema kutoa misaada ya chakula kwa wanaohitajia ni katika mafundisho ya Kiislamu.  Msimamizi wa chekechea hiyo, Bi. Saeeda Aslam anasema njaa haibagui. Katika mwezi wote wa disemba Waislamu wamekusanya karibu tani 10 za misaada kote Liverpool na miongoni mwa maeneo ambayo misaada imekusanywa ni katika Msikiti wa Abdullah Quillam uliojengwa mwaka 1887.

Stepehen Middleton mwanaharakati ambaye alikusanya misaada iliyokuwa katika chekechea ya Happy Nursery anasema binafsi ana uzoefu kwani aliwahi kutegemea misaada ya chakuka na anasima misaada hiyo ni muhimu sana kwani kuna idadi kubwa ya watu wasio na uwezo wa kujipatia chakula mjini Liverpool.

3467517

Name:
Email:
* Comment: