IQNA

11:55 - January 01, 2019
News ID: 3471793
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe wa pongezi viongozi na mataifa ya Wakristo kwa munasaba wa kuanza mwaka mpya wa 2019 Miladia.

Rais Rouhani amewatakia Wakristo nchini Iran na kote duniani mwaka mpya wenye baraka, utulivu na amani.

Rais wa Iran ameongeza kuwa uzawa wa Nabii Isa AS (Yesu) uliwaletea wanadamu umaanawi, amani, na urafiki. Ameongeza kuwa, anataraji mwaka mpya utapelekea kushuhudiwa amani zaidi,uadilifu, kuangamizwa kila aina ya maadili mabovu na ubaguzi.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif naye pia ametuma ujumbe wa kheri na fanaka kwa munasaba wa kuanza mwaka mpya wa 2019 Miladia.

Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter Jumatatu usiku, Zarif amewatakia watu wote duniani kutoka kila rangi, dini na kaumu mwaka mpya uliojaa afya, amani na utulivu.

3467582

Name:
Email:
* Comment: