IQNA

11:50 - January 02, 2019
News ID: 3471795
TEHRAN (IQNA)-Wakuu wa utawala wa China wamefunga misikiti mitatu katika mji wa Weishan katika mkoa wa Yunnan kusini mwa nchi hiyo.

Misikiti hiyo ya Waislamu wa jamii ya Hui imefungwa baada ya wakuu wa eneo hilo kudai kuwa ilikuwa ikitoa mafunzo ya kidini yaliyo kinyume cha sheria.

Mkanda wa video ulioenea mitandaoni unaonyesha maafisa wa polisi wakikabiliana na Waislamu wa jamii ya Hui ambao walikuwa wakijaribu kuzuia msikiti huo kufungwa.

Waislamu wa kabila la Hui wanakadiriwa kuwa 700,000 katika mkoa wa Yunnan.

Kuna makabila 10 ya Waislamu kati ya makabila yote 56 nchini China. Makabila ya Waislamu ni pamoja na Wahui, Wauyghur, Wakyrgyz,Wakazakh, Watajik, Watatar, Wauzbeki, Wasalar, Wabao'a na Wadongshing na aghalabu wanaishi kaskazini na kaskazini mashariki mwa China.

Utawala wa China unaendelea kupuuza malalamiko ya dunia kuhusu kuendelea kuteswa Waislamu waliowachache nchini humo.

3467598

Name:
Email:
* Comment: