IQNA

10:51 - January 03, 2019
News ID: 3471796
TEHRAN (IQNA)- Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar kimetangaza masharti kwa wanaotaka kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yanayaondaliwa na chuo hicho katika mwaka huu wa 1440 Hijria Qamaria.

Katika taarifa, Al Azhar imesema mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yatafanyika katika vitengo vitano tafauti.

Taarifa hiyo imesema wanaolenga kushiriki katika mashindano hayo wanaweza kutumbelea tovuti ya : http://azhar.eg/quranregister kwa maelezo zaidi.

Washiriki kutoka nje ya Misri katika mashindano hayo wanatakiwa kufika katika vituo vya Kiislamu ambavyo vinasimamiwa na Al Azhar ili kujisajili.

Muhula wa mwisho wa kujisajili ni katika mwisho wa mwezi wa Jumaada al-Akhir. Aidha mchujo wa washiriki wa mashindano hayo umepengwa kufanyika katika miezi ya Jumaada al-Akhir na Rajab ambapo awamu ya kwanza ya mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani imepengwa kufanyika kuanzia tarehe 15 hadi 22 mwezi wa Shaaban.

Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Al Azhar imepangwa kufanyika kati ya tarehe 23 na 28 Shaaban na Saba Ramadhani kutafanyika sherehe za kuwaenzi na kuwatunuku zawadi washindi.

3778076

Name:
Email:
* Comment: