IQNA

Maandamano ya 'Siku ya Ardhi" yalianza mwaka 2018 kwa munasaba wa mwaka wa 42 wa siku hiyo huko Palestina. Maandamano ya amani ya "Haki ya Kurejea" yalianza tarehe 30 Machi katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza na hadi sasa yanaendelea.

Siku ya ardhi hukumbusha uamuzi wa kidhalimu uliochukuliwa na utawala wa Kizayuni tarehe 30 Machi 1976 kuhusiana na kuzipora na kuzihodhi ardhi za Wapalestina.

Mnamo Mei 14 mwaka 2018, sambamba na kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Quds Tukufu (Jerusalem) idadi kubwa ya Wapalelestina waliokuwa wakiandamana kulalamikia hatua hiyo waliuawa shahidi na kujeruhiwa.