IQNA

Kongamano la Kimataifa la Kiislamu nchini Misri lajadili misimamo mikali, ugaidi

20:51 - January 20, 2019
Habari ID: 3471812
TEHRAN (IQNA)- Kongamano la Kimataifa la Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu limefanyika nchini Misri na kuwaleta pamoja wawakilishi wa nchi 40.

Kwa mujibu wa taarifa, kongamano hilo la siku mbili lilifunguliwa Jumamosi katika sherhee iliyodhudhuriwa na Waziri wa Wakfu wa Misri Sheikh Mukhtar Gomaa. Kwa ujumla mkutano huo ulikuwa na wajumbe 150 kutoka nchi 40 zikiwemo Sudan, Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia. Miongoni mwa washiriki walikuwemo mawaziri wa masuala ya Kiislamu kutoka nchi 13.

Katika kongamano hilo kuliwasilishwa makala 50 za utafiti kuhusu misingi ya kidini, utaifa, na elimu. Aidha kongamano hilo limekadili nafasi ya familia na vyombo vya habari katika malezi na halikadhalika mikakati ya mazungumzo ya kidini kwa lengo la kuzuia ugaidi na misimamo mikali. Washiriki katika mkutano huo walisisitiza kuhusu malezi bora ili kuzuia ugaidi na misimamo mikali katika jamii za Waislamu duniani.

Kongamano hilo pia limeandaa warsha maalumu kuhusu uhusiano wa Misri na nchi za Afrika na nafasi ya familia katika kuleta uthabiti wa kijamii na kuwalinda vijana ili wasitumbukie katika misimamo mikali ya kidini.   

3467735

captcha