IQNA

Marekani yalazimika kumuachilia huru Bi. Hashemi wa Press TV

10:11 - January 24, 2019
Habari ID: 3471818
TEHRAN (IQNA)- Hatimaye utawala wa Marekani umelazimika kumuachulia huru bila kumfugulia mashtaka mtangazaji wa Press TV, Bi. Marzieh Hashemi baada ya kumshikilia kizuizini kinyume cha sheria kwa muda wa siku 11.

Katika taarifa, familia yake  imesema Bi. Hashemi ameachiliwa huru mjini Washington DC pasi na kufunguliwa mashtaka. Jana Jumatano alifika mbele ya Jopo la Mahakama lenye wanachama 23 na duru zinasema aliachiliwa baada ya ushahidi wake kusikilizwa.

Taarifa ya familia yake imesema. Bi Marzieh Hashemi ametoa wito kwa watu wote duniani kuendeleza maandamano ya kupinga mfumo wa sheria nchini Marekani. Taarifa hiyo imesema, 'kama ambavyo Wamarekani wanafahamu watu weusi wanakandamizwa nchini humo, hivi sasa Wamarekani pia wanapaswa kuzungumza kuhusu namna Polisi ya Upelelezi Marekani, FBI, inavyowakandamiza Waislamu." Taarifa hiyo imesema Bi. Marzieh Hashemi atashiriki katika maandamano makubwa mjini Washington DC siku ya Ijumaa na kuongeza kuwa, kadhia si ya Bi. Hashemi pekee, bali inahusu kila mtu, Mwislamu na asiyekuwa Mwislamu anaweza kushikiliwa korokorini Marekani bila kufahamishwa makosa yake.

Wakati huo huo Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB, Dkt. Peyman Jebeli amesema Marekani imelazimika kumuachilia huru Bi. Hashemu kutokana na mashinikizo ya fikra za umma. Amesema kuna haja ya kuzidi kushadidisha harakati za kuamsha fikra za umma nchini Marekani ili nchi hiyo iwaachilie wale wote inaowashikilia kinyume cha sheria. Aidha amesema kuachiliwa huru Bi. Hashemi ni mafanikio makubwa kwa vyombo huru vya habari hasa televisheni za Press TV na Al Alam.

Bi. Marzieh Hashemi, Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika, anayefanya kazi na Televisehni ya Press TV ya hapa Tehran ambaye alikuwa akiitwa Melanie Franklin kabla ya kusilimu, alitiwa nguvuni Jumapili ya tarehe 13 Januari katika Uwanja wa Ndege wa St. Louis, Missouri na kupelekwa mjini Washington DC alikoshikiliwa kwa muda wa siku 11.

Akiwa korokoroni, Marzieh Hashemi alivuliwa hijabu yake na kulazimishwa kula nyama ya nguruwe ambayo ni haramu kwa Waislamu, kitendo ambacho ni ukiukwaji wa wazi wa matukufu na thamani za Kiislamu. Aidha mbali na kumnyima chakula halali, wakuu wa Marekani pia walikataa kumpa Bi. Hashemi nguo zinazofaa katika msimu huu wa baridi kali nchini humo.

Hatua ya Marekani kumshikilia Bi. Hashemi imelaaniwa vikali kote duniani ambapo kumefanyika maandamano mbali mbali ya kutaka aachiliwe huru. Aidha kumekuwepo kampeni za kumuunga mkono Bi. Hashemi katika mitandao ya kijamii.

3784008

captcha