IQNA

Kiongozi Muadhamu Azuru Haram ya Imam Khomeini MA na Maziara ya Mashahidi

13:23 - January 30, 2019
Habari ID: 3471825
TEHRAN (IQNA)- Katika wakati huu wa kukaribia maadhimisho ya miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mapema leo asubuhi mjini Tehran amefanya ziara katika Haram toharifu ya Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na mbali na kuswali katika Haram hiyo na kumsomea Faatiha, amemuombea dua za kheri mwanachuoni huyo mkubwa wa zama hizi.

Aidha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezuru maziara ya mashahidi  wakubwa kama vile mashahidi Beheshti, Rajai, Bahonar na mashahidi wengine wa tukio la tarehe 7 Tir na kuwaombea dua za kheri ili Mwenyezi Mungu awapandishe daraja za juu waja wake hao wema.

Baada ya hapo Ayatullah Khamenei amefanya ziara katika maziara ya mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wa vita vya kujihami kutakatifu, mashahidi wa kulinda Haram na mashahidi wa Hija na kumuomba Allah azipe utulivu na kila la kheri roho za wapigania haki hao, amemuomba Mwenyezi Mungu azidi kulipa ushindi taifa kubwa la Iran katika wakati huu wa kukaribia kuingia kwenye muongo wa tano wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu huanza tarehe 12 Bahman (Februari 1) kila mwaka na kuendelea kwa muda wa siku 10 maarufu kwa jina la Alfajiri Kumi. Tarehe 22 Bahman (Februari 11) ndiyo siku zinapofikia kileleni sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran.

3785749

captcha