IQNA

Uingereza yaendelea kuiuzia Saudia silaha licha ya jinai zake Yemen

22:24 - February 12, 2019
Habari ID: 3471838
TEHRAN (IQNA)- Kamati ya Bunge la Uingereza ambayo ilikuwa na jukumu la kuchunguza mauzo ya silaha za nchi hiyo mwaka 2017 imelaaniwa vikali kwa kupuuza uuzaji wa silaha kwa Saudi Arabia nchi ambayo inawaua raia kiholela katika vita vya Yemen.

Kamati ya Udhibiti wa Mauzo ya Silaha Nje ya Nchi (CAEC) katika Bunge la Uingereza imekuwa ikichunguza ripoti ya mwaka 2017 ya serikali ya London kuhusu mauzo ya silaha na iliitisha kikao chake cha kwanza wiki iliyopita katika.

Hatahivyo kamati hiyo iloenekana kupuuza mauzo ya silaha za Uingereza kwa utawala wa Saudi Arabia. Hii ni katika hali ambayo Saudia ni mnunuzi mkubwa zaidi wa silaha za Uingereza tokea mwaka 2015, mwaka ambao ilianzisha hujuma dhidi ya nchi jirani na masikini ya Yemen.

Watetezi wa haki za binadamu wamehoji ni kwa nini kadhia ya Yemen imepuuzwa huku kukiwa na wasiwasi kuwa serikali ya Waziri Mkuu Theresa May haitaki kuweka wazi biashara ya silaha na Saudia. Katika ripoti iliyopita, wabunge wengi walitaka serikali iache kuizuia Saudia silaha kutokana na jinai za utawlaa huo.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi. Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasiopungua 15,000 wasio na hatia. Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha katika vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani, Uingereza  na utawala haramu wa Israel. Hivi karibuni Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Watoto, Save The Children, lilitangaza kuwa watoto zaidi ya 84,700 wa Yemen wamepoteza maisha kutokana na makali ya njaa na utapiamlo, tangu Saudi Arabia ianzishe vita dhidi ya nchi hiyo maskini jirani yake zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, ripoti mbalimbali za Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) zimekuwa zikitahadharisha kuhusiana na matokeo mabaya na maafa yanayosababishwa na kuendelea hujuma ya kijeshi ya Saudi Arabia na washirika wake huko nchini Yemen.

Aidha ripoti mbalimbali zinaeleza kwamba, zaidi ya watoto milioni 11 wa Yemen wanakabiliwa na uhaba wa chakula, maradhi na ukosefu wa makazi.

3467910

captcha