IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya walemavu wa macho yafanyika Iraq

13:06 - February 13, 2019
Habari ID: 3471840
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya Kitaifa ya Walemavu wa Macho yamemalizika Jumatatu wiki hii nchini Iraq.

Mashindano hayo ya Qur'ani yaliandaliwa na Taasisi ya Sayansi za Qur'ani inayofungamana na Idara ya Wakfu ya Waislamu wa Madhehebu ya Shia Iraq.

Mashindano hayo yalikuwa na washiriki 25 waliofika fainali katika kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur'ani kutoka maeneo mbali mbali ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Kwa mujibu wa jopo la majaji, Muhammad Ali Kumash alishinda kategoria ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu.

Katika kategoria ya qiraa au kusoma Qur'ani, Qassim Sabah Nouri, Ridha Tali Nasser na Sajjad Ala walishika nafasi ya kwanza hadi ya tatu kwa taratibu.

Waliochukua nafasi za kwanza na za pili katika kategoria zote mbili wataiwakilisha Iraq katika Mashindano ya Nne ya Kimataifa ya Qur'ani ya Walemavu wa Machi ambayo yamepangwa kufanyika Tehran mwezi Aprili.

3789394

captcha