IQNA

Kubuni ajira kupitia sanaa ya mkono

Ingawa biashara ya sanaa za mkono imepungia ikilinganishwa na miaka ya nyuma, lakini bado kuna wale ambao wanaendelea kutegeneza bidhaa mbali mbali kwa mikono. Sekta ya sanaa ya mkono katika eneo la Khuzestan kusini magharibi mwa Iran imepata ilhamu kutoka historia ndefu ya eneo la Zagros ambalo ni susu au chimbuko la ustaarabu na utamaduni wa Waelami. Uwepo wa kaumu na tamaduni mbali mbali kama vile za Wabakhtiari na Waarabu ni jambo ambalo limeibua anuai ya sanaa ya mkono katika eneo hilo. Picha hizi hapa zinaonyesha namna Kamati ya Imam Khomeini MA ya Kutoa Misaada inavyobuni nafasi za ajira miongoni mwa wanawake