IQNA

Serikali ya Sudan yasisitiza kuunga mkono Madrassah za Qur'ani

11:44 - March 06, 2019
Habari ID: 3471864
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Sudan imetangaza azma yake ya kuunga mkono madrassah za Qur'ani nchini humo ili kuhakikisha zinafanikiwa katika kustawisha elimu ya Qur'ani.

Hayo yamedokezwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Sudan Osman Mohamed Yousif Kibir katika sherehe iliyofanyika Jumapili mjini Khartoum iliyopita kuwaenzi wanafunzi 150 waliohitimu katika vyuo vya kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini humo.

Aidha alipongeza jitihada ambazo zimefanyika kutumia uzoefu wa madrassah za kisasa na zile za jadi. Halikadhalika Kibir ametoa wito kwa watu wote wa Sudan kuzingatia na kulipa uzito mkubwa suala la kuwafunza watoto wao Qur'ani Tukufu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh Muhammad Abdul Razzaq, Mkuu wa Idara ya Zakati nchini Sudan amesema idara yake inaunga mkono madrassah 2800 za Qur'ani katika nchi hiyo.

Harakati za Qur'ani nchini Sudan zimeenea sana na watu hulipa uzito mkubwa suala la kusoma Qur'ani.

3468053

captcha