IQNA

Wanafunzi wa chekechea za Kikristo Ujerumani kufunzwa Uislamu

22:17 - March 12, 2019
Habari ID: 3471872
TEHRAN (IQNA)- Watoto wa shule moja ya chekechea ya Wakristo mjini Dusseldorf nchini Ujerumani wataanza kufunzwa Uislamu.

Kwa mujibu wa taarifa, mpango huo wa kufunza Uislamu kwa watoto umeandaliwa na kasisi wa kanisa moja la walokole mjini humo. Kanisa hilo linasema iwapo watoto watafahamu mafunzo ya dini zinginezo basi wanaweza kuishi maisha ya amani na maelewano na hilo ni muhimu kwa mustakabali wa nchi.

Kwa mujibu wa mpango huo, Imamu wa msikiti mjini humo amepewa jukumu la kuwaelezea watoto wa chekechea kuhusu itikadi za Kiislamu.

Wawakilishi wa makanisa mawili makubwa Dusseldorf wanasema watoto hao watafunzwa kuhusu nukta nyingi za pamoja na Ukristo wa Kiprotestanti na Uislamu. Mpango huo  unatazamiwa kuanza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

3797246

captcha