IQNA

Shule ya Waislamu yahujumiwa, Qur'ani yavunjiwa heshima Newcastle, Uingereza

15:19 - March 28, 2019
Habari ID: 3471891
TEHRAN (IQNA)- Shule ya Waislamu mjini New Castle Uingereza imehujumiwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu ambao walivunjia haeshima nakala za Qur'ani Tukufu katika shule hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa Akademia ya Bahr mjini Newcastle ilihujumiwa Jumatatu jioni hii ikiwa ni mara ya pili shule hiyo kulengwa katika kipindi cha miezi mitatu.

Mkuu wa shule hiyo, Imam Abdul Muheet amesema genge lililohujumu shule hiyo na kuvunja madirisha kabla ya kuchana nakala za Qur'ani na kuzitupa sakafuni.

Amesema alipigiwa simu na kufika shuleni hapo kabla ya wahalifu hao kuondoka na aliwasikia wakisema eti Waislamu ni magaidi.

Tukio hilo la Newcastle limekuja siku chache baada ya misikiti 5 kushambuliwa katika mji wa New Castle nchini Uingereza.

Watu wawili walitiwa mbaroni kufuatia mashambulizi hayo yaliyokuja chini ya wiki moja baada ya gaidi kushambulia misikiti mjini Christchurch New Zeland na kuwaua shahidi zaidi ya Waislamu 52.

Aliyefanya unyama huo ni Brenton Tarrant, gaidi mwenye chuki na Uislamu mwenye uraia wa Australia. Gaidi Tarrant ni mfuasi sugu wa  Rais Donald Trump wa Marekani ambaye ni mashuhuri kwa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

3468194

captcha