IQNA

Bustani ya Qur'ani Yazinduliwa Dubai

21:15 - March 30, 2019
Habari ID: 3471894
TEHRAN (IQNA)-Bustani ya Qur'ani imezinduliwa Ijumaa katika Umoja wa Falme za Kiarabu mjini Dubai katika eneo la Al Khawaneej Ijumaa ambapo wageni watapa fursa ya kujifunza kuhusu miujiza ya Qur'ani Tukufu.

Lengo kuu la kuanzishwa bustani hiyo limetajwa kuwa ni kuwaleta pamoja watu wa tamaduni, dini na kaumi mbali mbali ili waweze kuona mafanikio ya Uislamu katika uga wa ekolojia ya mimea.

Bustani hiyo imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekari 60 na mimea yote iliyoko hapo imetajwa katika Qur'ani Tukufu. Aidha bustani hiyo ina vivutio vingine kama vile maeneo ya watoto kucheza, Kona ya Umrah, jukwaa la wazi la tamthilia, na maeneo yanayoonyesha miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu.

Manispaa ya Dubai imetangaza kuwa hakuna malipo yoyote kwa anayetaka kutembelea bustani hiyo.

3468203

captcha