IQNA

Wakuu wa China wabomoa msikiti eneo la Gansu

23:20 - April 20, 2019
Habari ID: 3471922
TEHRAN (IQNA)- Msikiti umebomolewa katika mkoa wa Gansu, kaskazini-kati mwak China ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kufuta turathi za Kiislamu nchini humo.

Duri zinadokeza kuwa, mnamo Aprili 9 2019, maafisa wa utawala wa China walibomoa sehemu ya msikiti ulio katika kijiji cha Gazhuang katika eneo la Linxia Hui mkoani Gansu. Katika oparesheni hiyo , maafisa wa utawala walibomoa kuba la dhahabu la msikiti na pia naqshi za Kiislamu katika msikiti huo.

Msikiti huo mpya ulifunguliwa mwezi moja uliopita na wakaazi walitahadahrishwa wasichukua picha za tukio hilo. Pamoja na hayo, video za msikiti uliobomolewa zimeenea katika mitandao ya kijamii huku winchi iliyotumika katika kubomoa msikiti ikiwa inaonekana.

Taarifa zinasema oparesehni za kubomoa misikiti zilianza mkoani Gansu mwaka jana. Baadhi ya misikiti imebomolewa kikamilifu na katika misikiti mingine ni kuba na minara inayobomolewa huku maandishi yote ya kiarabu yakifutwa.

Hivi karibuni pia picha za satalaiti zilionyesha kuwa serikali ya China inabomoa misikiti muhimu ya eneo lenye Waislamu wengi la Xinjiang.

Wanaharakati wanasema picha za satalaiti za kabla na baada zinaonyesha kuwa kwa uchache misikiti miwili muhimu na mikubwa imebomolewa katika eneo la Xinjiang. Kati ya misikiti iliyobomolewa ni Msikiti wa Keriya Aitika uliojengwa miaka 800 iliyopita na ambao uliwekwa katika Turathi za Usanifu Majengo China mwaka 2017. Ripoti pia zinasema utawala wa China umebomoa Msikiti wa Kargilik katika eneo hilo.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeongezeka sera za kuwakandamiza Waislamu katika nchi hiyo hasa katika jimbo la Xinjiang lenye Waislamu Zaidi ya milioni 10 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na misimamo mikali.

3805129

captcha