IQNA

Spika wa Bunge la Iran

Ulimwengu wa Kiislamu unakabiliwa na tatizo la misimamo mikali na utakfiri

20:06 - April 28, 2019
Habari ID: 3471931
TEHRAN (IQNA) -Spika wa Bunge la Iran, Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, ulimwengu wa Kiislamu leo unakabiliwa na tatizo la misimamo mikali na utakfiri.

Ali Larijani, Spika wa Bunge la Iran ameyasema hayo Jumapili mjini Tehran katika kongamano la kimataifa la 'Mustakabali wa Ulimwengu katika Dira ya Mwaka 2035' ambapo ameashiria hujuma za kigaidi Sri Lanka na kunyongwa kwa umati raia 37 wa Saudi Arabia. Ameutahadahrisha utawala wa Saudia kutokana na hatua yake hiyo ya kuwanyonga raia hao.

Larijani ameendeleza hotuba yake kwa kusema: "Iran, Malaysia, Uturuki na Iraq zinapaswa kuweka msingi wa ushirikiano wa kibiashara ili nchi zingine za Kiislamu zijiunge na harakati hiyo na kwa msingi huo kuundwe mazingira mapya ya mawasiliano ya kiuchumi baina ya nchi hizo za Kiislamu.

Spika wa Bunge la Iran pia amesema kuna haka ya kuwa na Mahakama ya Upatanishi ya Kiislamu ili iwezi kutumiwa na nchi za Kiislamu katika masuala ya kibiashara n.k.

Larijani ameongeza kuwa  Wairani kwa kusimama kwao kidete watapelekea watawala wa Marekani wajute. Ameashiria tabia za rais wa Marekani na kusema: "Trump anadhani hatua anazochukua ni kwa maslahi ya Marekani lakini sera zake hizo zitapelekea ulimwengu usiiamini tena Marekani."

Spika wa Bunge la Iran ameashiria kujiondoa Marekani katika baadhi ya mikataba ya kimataifa ukiwemo Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Paris, na mapatano ya nyuklia ya Iran ya JCPOA na kusema: "Inasikitisha kuwa Umoja wa Ulaya umeonyesha kuwa hauna nguvu za kutosha za kulinda na kutetea mikataba hiyo ya kimataifa."

Larijani ameashiria kadhia ya Marekani kujiondoa katika JCPOA na kadhia ya nyuklia ya Iran na kusema hatua hiyo ni misdaki ya kutoaminika Marekani katika mikataba ya kimataifa ambayo yenyewe inatia saini. Aidha amesema Iran haija shuhudia nchi za Ulaya zikichukua hatua zozote za kivitendo kulinda JCPOA na mikataba mingine ya kimataifa.

3806956

captcha