IQNA

Mipango 126 mipya ya ubunifu katika maonyesho ya kimataifa ya Qur’ani Tehran

11:07 - May 13, 2019
Habari ID: 3471954
TEHRAN (IQNA) – Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran mwaka huu yana mipango 126 ya ubunifu katika sekta ya Qur’ani na hivyo kuyafanya yawe ya kipekee.

Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho hayo siku ya Jumamosi, Bw. Abdul Hadi Faqihzadeh, Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani Tukufu aidha amesema: “Maonyesho ya mwaka huu pia yameimarika zaidi katika uga wa kitaifa na kimataifa ikilinganishwa na miaka iliyopita. Taasisi nyingi zaidi za kiutamaduni na za wananchi zimeshiriki katika maoneysho haya.”

Bw. Abdul Hadi Faqihzadeh ambaye pia ni msimamizi wa maonyehso hayo amesema kuwa mwaka huu kuliwasilishwa mipango 700 ya kutekelezwa katika maonyesho hayo na baada ya uchunguzi wa kina mipango 126 iliidhinishwa. Ameongeza kuwa maonyesho yam waka huu yataendelea hadi tarehe 19 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Halikadhalika Bw. Faqihzadeh amesema mwaka huu maonyesho hayo yamezivutuia taasisi za Qur’ani kutoka nchi kadhaa za Kiislamu na kwamba nchi 10 zinashiriki  katika maonyesho hayo.

3810641

captcha