IQNA

Jeshi la Kizayuni lawajeruhi Wapalestina waliokuwa katika maandamano ya amani Ghaza

19:41 - August 31, 2019
Habari ID: 3472107
TEHRAN (IQNA) – Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limewafyatulia risasi na kuwajeruhi makumi ya Wapalestina waliokuwa wakiandamana kwa amani katika Ijumaa ya 72 ya maandamano ya 'Haki ya Kurejea' huko katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa taarifa, Wapalestina 75 wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi katikka maandamano ya jana ya "Haki ya Kurejea' katika maeneo ya mpakani ya Ukanda wa Ghaza. Kaulimbiu ya maandamano ya wiki hii ilikuwa ni "Utiifu kwa Mashahidi.

Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel waliwafyatulia risasi hai na kuwarushia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji wa maandamano ya 'Haki ya Kurejea".

Maandamano ya "Haki ya Kurejea" ya kupigania Wapalestina kurejea katika ardhi za mababu zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel yalianza tarehe 30 Machi 2018 siku ambayo ilisadifiana na kumbukumbu ya "Siku ya Ardhi" huko Palestina. Maandamano hayo hufanyika kila Ijumaa katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza na maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na utawala bandia wa Israel.

Siku ya Ardhi inayoadhimishwa kila mwaka huko Palestina ni kumbukumbu ya uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kuteka ardhi za Wapalestina tarehe 30 Machi 1976 na kuziingiza ardhi hizo katika maeneo mengine ya Wapalestina ambayo imekuwa ikiyakalia kwa mabavu tangu mwaka 1948.

Hadi leo hii utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuteka ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa lengo la kufuta kabisa utambulisho wake wa Kiislamu-Kipalestina na mahala pake kuupachika utambulisho bandia ya Kizayuni. Wapalestina wameama kuendeleza mapambano ya kukomboa ardhi zao.

3469285/

captcha