IQNA

Mijumuiko ya "Watoto Wanaonyonya wa Hussein" yafanyika kimataifa

21:20 - September 06, 2019
Habari ID: 3472117
TEHRAN (IQNA) - Mijumuiko ya Kimataifa kwa jina la "Watoto Wachanga Wanaonyonya wa Hussein AS" imefanyika leo Ijumaa katika zaidi ya maeneo elfu sita katika Iran ya Kiislamu na katika nchi 45 duniani sambamba na Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Muharram.

Mijimuiko hiyo kimataifa ya iliyopewa jina la ' Watoto Wachanga wanaonyonya wa Imam Hussein AS' inafanywa na Waislamu duniani ikiwemo hapa Iran, India, Pakistan, Iraq, Saudia, Uturuki na Afghanistan katika Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Muharram katika kuwakumbuka watoto waliouliwa shahidi katika Siku ya Ashura.
Katika mijumuiko hiyo, akina mama huwavalisha watoto wao wanaonyonya maziwa mavazi yenye kufanana na kisha huwafunga vipande vya vitambaa kichwani vilivyoandikwa jina tukufu la Ali Asghar AS; na hivyo kudhihirisha mapenzi na kujitolea kwao kwa familia hiyo tukufu na adilifu.
Mtukufu Ali Asghari AS alikuwa mtoto mdogo zaidi wa Imam Hussein a.s; Imamu wa tatu wa Waislamu wa Kishia ambaye aliuliwa shahidi tarehe Sita Muharram mwaka 61 Hijria huko Karbala akiwa na umri wa miezi sita.

Itakumbukwa kuwa tarehe 10 Muharram miaka 1380 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria Qamaria, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili ili kuilinda dini ya Allah na hatimaye waliuawa Shahidi.

3840366/

captcha