IQNA

Wenye ulemavu wa macho wapata Kituo cha kuhifadhi Qur'ani nchini Russia

11:52 - September 19, 2019
Habari ID: 3472138
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu maalumu kwa watu wenye ulemavu wa macho kimefunguliwa nchini Russia katika eneo la Dagestan mapema wiki hii.

Sherehe za kufungua kituo hicho zimefanyika Jumatatu na kuhudhuriwa na Mufti wa Jamhuri ya Dagestan Sheikh Ahmad Afandi ambaye amewapongeza wote kwa mafanikio yaliyopatikana.

Aidha amewatakia taufiki wanafunzi huku akibainisha matumaini yake kuwa kituo hicho kitaweza kukidhi haja ya wale wote wanaotafuta elimu hata kama wana ulemavu.

Kituo hicho kinalenga kutoa mafunzi kwa wanawake na wanaume huku kipaumbele kikiwa ni kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa njia sahihi. Aidha wanafunzi katika kituo hicho wataweza kusoma masomo mengine yasiyo ya kidini.  Kwa wale wenye ulemavu wa macho, kufunguliwa kituo hicho ni chimbuko cha furaha kubwa. Washiriki walimshukuru Mufti Afandi kwa kuanzisha kituo hicho na kusema ni fursa ya kupata elimu. Hii n mara ya pili kwa Mufti wa Dagestan kuanzisha kituo cha kuwasaidia watu wenye ulemavu. Hivi karibuni kulifunguliwa kituo cha Kiislamu cha wenye uziwi katika mji mkuu wa Dagestan, Makhachkala. Kituo hicho cha kuhifadhi Qur'ani maalumu kwa watu wenye ulemavu wa macho pia kimefunguliwa mjini Makhachkala.

Hivi sasa kuna idadi kubwa ya Waislamu duniani wenye ulemavu wa macho ambao wanajitahidi kuhifadhi Qur'ani kikamilifu kwa kutegemea misahafu iliyoandikwa kwa maandishi ya nukta nundu au Braille.

3843166

captcha