IQNA

Palestina yaishukuru Jordan kwa kuwasaidia mahujaji wake

10:59 - December 03, 2008
Habari ID: 1715250
Wakuu wa Kamati ya Hija na Umrah ya Palestina wamekutana na Waziri wa Waqfu na Masuala ya Dini wa Jordan, Abdulfattah Salah ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Hija ya nchi hiyo na wametoa shukrani zao za dhati kwa juhudi za Jordan katika kuwapa himaya mahujaji wa Palestina.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Makka, Mkuu wa Kamati ya Hija na Umrah ya Palestina , Salim Shlatah amesema kuwa wanaishukuru serikali ya Jordan kwa ajili ya huduma zake kwa mahujaji wa Palestina ambazo zimewawezesha kutekeleza amali za Hija.
Amemshukuru kwa dhati Mfalme Abdullah wa Jordan kwa tadbiri yake kuhusiana na suala hili na kuongeza kuwa wanaishukuru sana Wizara ya Wafu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan ambayo kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikishughulikia masuala ya Hija na Umra ya Wapalestina.
Katika mkutano huo uliofanyika hivi karibuni katika mji mtakatifu wa Makka, Waziri wa Waqfu wa Jordan ameelezea furaha yake kuwa mahujaji wa Palestina wameridhika na kuongeza kuwa: wanawajali mahujaji wa Palestina kama wanavyowazingatia mahujaji wa Jordan. Mwishoni mwa mkutano huo amewatakia mahujaji wa Palestina afya njema na amemuomba Mwenyezi Mungu awatakabalie ibada yao ya Hija.
328908

captcha