IQNA

Al Azhar yapinga kuakhirishwa Hijja na Umrah

15:58 - May 16, 2009
Habari ID: 1778919
Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri tarehe 14 Mei imetoa taarifa na kupinga kuakhirishwa safari za Hijja na Umrah kwa kisingizio cha kuonekana ishara za homa ya nguruwe katika eneo la Mashariki ya Kati.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan la Saudi Arabia, Mufti wa Misri Sheikh Ali Juma tarehe 13 Mei alitoa taarifa na kuwataka Mamufti na Maulamaa wote wa Kiislamu duniani kutoa fatwa ya pamoja ya kuwataka Waisalmu kuakhirisha safari za Hiija na Umrah kwa sababu ya kuibuka homa ya nguruwe. Taarifa hiyo imepingwa na Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar.
Mohammad Sayyid Tantawi, Sheikh Mkuu wa al Azhar amesema: "Hadi sasa hakuna ombi lolote lililotolewa na Wizara ya Afya ya Misri au nchi nyinginezo za Kiislamu zikitaka kutangazwe fatwa ya kisheria kuhusu kuakhirishwa safari ya Hijja au Umrah kwa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar".
Sheikh Tantawi ameongeza kuwa, Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar ndio chombo cha juu kabisa cha kidini nchini Misri na fatwa ya kuakhirisha safari ya Hijja au Umrah inapaswa kutokelewa tu na jumuiya hii kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu. 405356
captcha