IQNA

Nafasi ya vyombo vya habari katika kustawisha utamaduni wa Qur’ani

11:04 - January 01, 2012
Habari ID: 2248815
Kueneza misingi ya Qur’ani na kuimarisha utamaduni wa Qur’ani ni mambo ambayo yanahitaji kuakisiwa ipasavyo katika vyombo vya habari.
Haya ni kwa mujibu wa Sheikh Heydar al Mousawi, mkuu wa Kitengo cha Sayansi za Qur’ani katika Kitivo cha Fasihi cha Chuo Kikuu cha Dhi Qar nchini Iraq.
Katika mahojiano yake na IQNA, Sheikh al Mousawi amesema kuwa kuandaa makongamano ya Qur’ani ni hatua muhimu katika kueneza mafundisho ya Qur’ani Tukufu.
Akisisitiza umuhimu wa kuandaa vipindi vinavyofaa, ameelezea masikitiko yake kuwa vyombo vingi vya habari vya Iraq vimeshindwa kutengeneza vipindi vinavyovutia kuhusu kina cha mafundisho ya Qur’ani.
“Kanali ya Televisheni ya Al Kauthar (ya Iran inayorusha matangazo yake kote duniani) ni ya aina yake kwani ina vipindi vyenye thamani kuhusu Qur’ani Tukufu”, amesema.
Al Mousawi pia ameshukuru Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa IQNA lenye makao yake nchini Iran kwa ushirikiano wake na Taasisi ya Darul Qur’an Karim katika mji wa Nasiriya nchini Iraq hasa kuhusu kuandaa kongamano lenye anwani ya ‘Nafasi ya Vyombo vya Habari katika Kustawisha Utamaduni wa Qur’ani Iraq’.
924447
captcha