IQNA

Mashindano ya kujifunza Qur’ani Canada

14:43 - January 30, 2012
Habari ID: 2264901
Usajili wa washiriki katika Mashindano ya Nne ya Kila Mwaka ya Kujifunza Qur’ani Tukufu Mwaka 2012 umeanza katika jimbo la Quebec nchini Canada.
Kwa mujibu wa tovuti ya mosqueedequebec, mashindano hayo yanafanyika kwa himaya ya Msikiti wa Jamia wa Quebec na lengo limetajwa kuwa ni kuwahimiza na kuwatia motisha watoto na vijana Waislamu kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Mashindano hayo yamepangwa katika viwango vitatu vya utangulizi, kati na juu ambapo washiriki watajifunza qiraa na hifdhi ya Qur’ani Tukufu. Kabla ya kuingia katika darasa washiriki watafanyiwa mtihani wa kuainisha kiwango chao. Kila mwezi waliofanikiwa zaidi watatunikiwa zawadi.
Aidha mwishoni mwa mwaka wa Miladia washindi watatu kutoka viwango vyote vitatu watatunikiwa zawadi kama vile tiketi ya kwenda Umrah na zawadi za kifedha kuanzia dola 500 hadi 1000.
Mashindano hayo yatafanyika katika Msikiti wa Jamia wa Quebec.
943295
captcha