IQNA

FIBA yaondoa marufuku ya Hijabu kwa wachezaji wa kike basketboli

14:50 - August 29, 2015
Habari ID: 3353719
Shirikisho la Kimataifa la Basketboli FIBA limewaruhusi wachezaji wanawake Waislamu kuvaa Hijabu katika mechi za mchezo huo mashuhuri.

"Nina furaha kwani nimekuwa nikipigania kuvaa hijabu kwa sababu naamini ni haki," amesema mchezaji wa kulipwa wa basketboli kutoka Bosnia  Indira Kaljo.
Kaljo ameyasema hayo alipohojiwa na Shirika la Habari la Doğan wakati akiwa mjini Istanbul Uturuki alikowakilisha timu ya wanawake ya basketboli kutoka Saudia ya Jeddah United.
Mchezaji huo mwenye miaka 27 ni kati ya wachezaji wawili wa kike Waislamu ambao walitoa wito kwa FIBA Agosti mwaka jana kuondoa marufuku ya Hijabu wakati wa mechi.
FIBA imetoa matumaini mapya kwa wachezaji Waislamu baada ya kuruhusu wanawake wanaotaka kuvaa vazi la stara la Kiislamu kulivaa katika michezo rasmi. Hatua hiyo imepongezwa sana na wachezaji Waislamu. FIBA imesema marufuku hiyo imeondolewa kwa muda ili vazi hilo lifanyiwe majaribio na kwamba uamuzi kamili utachukuliwa mwaka 2016.../mh

3353579

captcha