Kwa mujibu wa tovuti ya tafsir.net, mashindano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani (HQMI) kwa ushirikiano na Taasisi ya Kiislamu na Kuhifadhi Qur'ani Bosnia.
Mashindano hayo yalifanyika katika Msikiti wa Gazi-Husrev-bey mjini Sarajevo ambapo kulikuwa na washiriki 53 wa kike na kiume.
Mashindano hayo yalikuwa na kategoria za kuhifadhi Qur'ani kikamilifu na pia kuhifadhi Juzuu 15 na tano.
Walioshika nafasi za juu walitunukiwa zawadi katika hafla iliyohudhuriwa na wasomi wa Qur'ani, Sheikh Hussein Samovich aliyewakilisha wanazuoni wa Kiislamu, Muhammad Ayat Mansour Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani na Nusrat Abdi Begovic mkurugenzi wa Elimu na Miongozo ya Kidini katika Kituo cha Kiislamu cha Bosnia.
Msikiti wa Gazi Husrev-bey ulijengwa karne ya 16 Miladia na ni mkubwa zaidi wa kihistoria Bosnia na Herzegovina ambao pia hutumika kama msikitu mkuu wa jamaa katika nchi hiyo ya Waislamu kusini mwa Ulaya.