IQNA

Mashindano ya Qur’ani katika Televisheni ya Algeria

14:31 - February 03, 2016
Habari ID: 3470110
Televisheni moja ya satalaiti nchini Algeria imetangaza mpango wa kuandaa mashindano ya Qur’ani.

Al Shuruq TV imesema mashindano hayo ni maalumu kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 15, imeripoti tovuti ya echoroukonline.com.

Imearifiwa kuwa mashindano hayo yatajumuisha kuhifadhi na qiraa ya Sura Ad Dhuhaa ya Qur’ani Tukufu.

Wanaotaka kushiriki wametakiwa kutoma faili la sauti ya qiraa yao kwa njia ya email.

Mshindi mshindi atatunukiwa zawadi ya safari ya wiki mbili ya Umrah katika mji mitakatifu ya Makkah na Madina.

Al Shuruq TV imewahi kuandaa mashindano ya kidini yanayojumuisha kuhifadhi Qur’ani na Hadhiti.

Algeria ni nchi ya Kiislamu-Kiarabu eneo la Kaskazini mwa Afrika na asilimia 99.7 ya wakaazi wake ni Waislamu.

3472196

captcha