IQNA

Mkutano wa OIC Jakarta, fursa ya Palestina Huru

11:06 - March 06, 2016
Habari ID: 3470183
Mchambuzi wa masuala ya mambo Muiondonesia amesema kikao kijacho cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta ni fursa kwa ajili ya uhuru wa taifa la Palestina.

Yun Shamoudi amesema kadhia ya Palestina ina umuhimu mkubwa na inapaswa kutatuliwa kwa haki na uadilifu.

Amesema wanachama wote wa OIC wana jukumu la kimaadili kujitahidi kuhakikisha kuwa kunaundwa taifa huru la Palestina.

Kikao cha 5 Kisicho cha Kawaida cha Viongozi wa OIC kuhusu Palestina na Qud Tukufu kinafanyika Machi 6-7 huko Jakarta Indonesia chini ya kauli mbiu ya "Umoja kwa ajili ya Suluhisho Adilifu”

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itawakilishwa katika kikao hicho na Waziri wa Mambo ya Nje Mohammad Javad Zarif.

Takwimu rasmi zinaonesha kuwa, tangu ilipoanza Intifadha ya Quds tarehe mosi Oktoba 2015 hadi hivi sasa, Wapalestina zaidi ya 185 wameshauawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi katili wa Israel katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Quds inayokaliwa kwa mabavu, Ukanda wa Ghaza na katika maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni tangu mwaka 1948. Zaidi ya Wapalestina 16 elfu wamejeruhiwa katika kipindi hicho. Vile vile tangu kuanza Intifadha ya Quds, karibu Wapalestina elfu 4 wametekwa nyara na Wazayuni na kupelekwa kusikojulikana.

Muda wote huu utawala wa Kizayuni umekuwa ukitumia mbinu mbalimbali za kuliangamiza kabisa taifa la Palestina ili ifike siku, asibakie mtu yeyote wala kipande chochote cha ardhi kitakachoitwa cha Wapalestina. Hata hivyo, wananchi wa Palestina wamesimama kidete kukabiliana na njama hizo. Hata huku kuongezeka idadi ya Wapalestina wanaouawa shahidi na kujeruhiwa katika Intifadha ya Quds, nako kunaonesha namna Wapalestina walivyosimama imara mikono mitupu, kukabiliana na jeshi la Israel lilijizatiti kwa kila aina ya silaha na kuwatangazia walimwengu historia na utambulisho wao wa kutokubali kudhulumiwa.

3459269

captcha