IQNA

Mwanazuoni wa Kisunni Uingereza

ISIS (Daesh) hawatafuatisha baina ya Shia na Sunni

13:36 - March 14, 2016
Habari ID: 3470196
Mwanazuoni wa Kisunni nchini Uingereza amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh halitafautishi baina ya Shia na Sunni katika kutekeleza jinai dhidi ya Waislamu.

Kwa mukibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Muhammad Umar ibn Ramadhan, mwenyekiti wa Taasisi ya Ramadhan Uingereza ameongeza kuwa Masunni wameathirika zadi ya Mashia katika jinai za kundi la kitakfiri la ISIS.

Akizungumza akiwa safarini nchini Iraq amesema: "Kile ambacho tumeshuhudia Iraq si vita vya kimadhehebu baina ya Wairaqi bali ni vita vya ISIS dhidi ya taifa la Iraq.”

Aidha amesema vijana 64 Waingereza wamejiunga na ISIS na kusema kunapaswa kufanyika uchugnuzi huru kuhusu ni kwa nini idadi kubwa ya vijana wa Ulaya wamejiunga na ISIS.

Sheikh Muhammad Umar ambaye anatembelea Iraq akiongoza ujumbe wa wanazuoni wa Kisunni kutoka Uingereza ili kupata maelezo kuhusu hali katika nchi hiyo inayokumbwa na vita. Aidha amefahamishwa kuhusu jitihada za kukabiliana na magaidi wakufurishaji hasa wa ISIS na nafasi ya wanazuoni na marajii taqlid wa Kishia katika kuwaleta Wairaqi pamoja ili wakabiliane na ugaidi.

Ujumbe huo wa Uingereza umetembelea pia haram takatifu za Imam Hussein AS na Hadhrat Abbas AS huko Karbala . Aidha wamtemebela haram takatifu za Imam Ali AS mjini Najaf, Imam Musa Kadhim AS Imam Javad AS huko Kadhimeyn pamoja na haram takatifu za Imam Hadi AS na Imam Hassan Askari AS huko Sammara kati ya maeneo mengine nchini Iraq.

Magaidi wa ISIS waliteka maeneo ya kaskazini na maghribi mwa Iraq mwaka 2014 wakitokea Syria ambako pia waliteka maeneo kadhaa. Hatahivyo kufuatia jitijada za Jeshi la Iraq na wapiganaji wa kujitolea ambao waliingia vitani kufuatia fatwa ya Ayatullah Ali al-Sistani, magaidi wa ISIS wamepata pigo kubwa.

3483122

captcha