IQNA

Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani chafunguliwa Ijara, Kenya

19:14 - June 28, 2016
Habari ID: 3470421
Shirika la Kutoa Misaada la Kutoa Misaada ya Kibinadamu Qatar (RAF) limefungua kituo kipya cha kuhifadhi kiitwacho "Al Rahmah" Qur'ani Tukufu kaskazini mashariki mwa Kenya.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kituo hicho cha Qur'ani katika eneo la Ijara kitaweza kutoa huduma za mafundisho ya kuhifadhi Qur'ani kwa takribani watu 20,000 wa eneo hilo na miji jirani.

Kituo hicho kina darasa tatu na maktaba na kinaweza kutoa mafunzo ya kuhifadhi Qur'ani kwa wasichana na wavulana 100 kwa wakati moja.

Aidha mbali na kuhifadhi Qur'ani wanafunzi pia wanajifunza kuhusu mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.

Kituo hicho kimeanzishwa kwa msingi wa mkakati wa 'Abwaab al Rahmah" ambao unahusu kuanzisha vituo vya Kiislamu na Qur'ani katika maeneo mbali mbali duniani kwa lengo la kukidhi mahitaji ya Waislamu wasiojiweza.

Shirika la Kutoa Misaada la Kutoa Misaada ya Kibinadamu Qatar (RAF) linasema vituo hivyo vina nafasi muhimu katika kutoa mafunzo ya Qur'ani na kulea kizazi kwa misingi ya mafundisho ya Qur'ani.

Waislamu wanakadiriwa kuwa karibu asilimia 35 ya wakaazi wote milioni 44 nchini Kenya huku wengi wakiwa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki, Pwani na pia mji mkuu Nairobi.

3510576

Kishikizo: kenya qurani iqna waislamu
captcha