IQNA

Magaidi wahujumu kaburi la mjukuu wa Mtume SAW, waua watu 40 Iraq

22:36 - July 08, 2016
Habari ID: 3470441
Magaidi wa ISIS Alhamisi walishambulia ziara la mjukuu wa Mtume Muhammad SAW katika mji wa Balad ulioko umbali wa kilomita 80 kutoka Baghdad na kuua watu wasiopungua 40.

Habari zinasema magaidi wa kundi hilo awali walishambulia kaburi la Sayyid Muhammad bin Ali al Hadi AS kwa maroketi na kisha magadi wengine watatu wakajiripua kwa mabomu katika lango kuu la kuingia kwenye haram hiyo suala lililopelekea kuuawa watu wasiopungua 40 na kujeruhi wengine zaidi ya 40 waliokuwa wakifanya ziara mahala hapo.

Kamanda wa operesheni ya Samurra Imad Zuhairi amesema magaidi wawili wa ISIS au Daesh wameaua katika uwanja wa haram hiyo wakijaribu kuingia ndani katika eneo hilo tukufu wakati wa Siku Kuu ya Idul Fitr. Amesema magadi hao walifyatua risasi ovyo mbele ya lango la haram hiyo na kusababisha moto mkubwa katika majengo na soko la kandokando yake.

Vilevile makundi ya wapiganaji ya wananchi yamemtia nguvuni gaidi mmoja wa kundi la ISIS aliyekuwa amejificha karibu na eneo hilo na kuua wengine kadhaa waliokuwa wakitoroka baada ya kushindwa kuingia ndani ya eneo hilo tukufu.

Shambulizila kuamkia leo katika mji wa Balad linafuatia lile la Jumapili iliyopita katika kitongoji cha Karrada mjini Baghdad ambalo limeua karibu watu 300. Kundi la kigaidi la ISIS limetangaza kuhusika na miripuko hiyo ya Baghdad.

3460330/40

Kishikizo: iraq isis au daesh iqna
captcha