IQNA

Serikali ya Nigeria yatakiwa kuwashtaki wanajeshi waliowaua Waislamu wa Kishia

10:36 - August 11, 2016
Habari ID: 3470516
Shirika moja la kutetea haki za binadamu Nigeria limetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuwafikisha kizimbani wanajeshi waliohusika katika kuwaua Waislamu wa madhehebu ya Shia mwezi Desemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kundi la ‘Access to Justice (A2J) limetoa wito kwa serikali ya jimbo la Kadun kuanzisha kesi dhidi ya maafisa wote wa kijeshi waliopatikana na hatia katika ripoti ya Jopo la Jaji Garba kuhusu mauaji ya wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Katika taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wake, Joseph Otteh, shirika hilo limesema serikali ya Jimbo la Kaduna inawashtaki watu 200 kwa mauaji ya mwanajeshi moja lakini haijafanya chochote kuhusu watu 348 waliouawa na jeshi jimboni humo.

Itakumbukwa kuwa tarehe 14 Disemba mwaka jana 2015, siku moja baada ya jeshi la Nigeria kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya Waislamu katika mji wa ZariaIkumbukwe kuwa kati ya Desemba 12-14 mwaka 2015, Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria IMN katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi lilidai kuwa wafuasi wa IMN walikuwa na jama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo. Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria hata hivyo inasisitiza kuwa zaidi ya Waislamu 1000 waliuliwa na jeshi la nchi hiyo katika hujuma hiyo.

Aidha Jeshi la Nigeria lilimkamata Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria akiwa pamoja na mke wake. Hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky inaripotiwa kuwa mbaya huku taarifa zikisema amepoteza jicho moja mbali na majeraha mengine mwilini. Serikali ya Nigeria inamshikilia kiongozi huyo wa Kiislamu tokea Desemba mwaka jana pasina kumfungulia mashtaka.

3460660


captcha