IQNA

Kiongozi wa Harakati wa Hizbullah

Saudi Arabia, Marekani ni waungaji mkono wakuu wa ugaidi katika eneo

13:13 - October 24, 2016
Habari ID: 3470632
Kiongozi wa Harakati wa Hizbullah ya Lebanon Sayyed Hassan Nasrallah amesema Saudi Arabia na Marekani ndio waungaji mkono wakuu wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh katika eneo.

Akizungumza, Jumapili mjini Beirut kwa mnasaba wa siku ya saba ya kuuawa kamanda wa Hizbullah  nchini Syria, Hatem Hamade, Sayyed Nasrallah amelaani vikali utawala wa Saudia kwa kuunga mkono magaidi wakufurishaji wa ISIS.

Ameongeza kuwa, email zilizovuja za waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani ambaye sasa ni mgombe kiti cha urais kwa tikiti ya Wademocrat, Hillary Clinton, ni ushahidi tosha kuwa Saudi Arabia na Marekani ni waungaji mkono wakuu wa ISIS.

Kuhusiana na hatua ya Hizbullah kuingia katikavita vya Syria kukabiliana na magaidi wa ISIS, Nasrallah amesema uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kuchunguza matukio yaliyoanzia Tunisia na kufika Syria.Saudi Arabia, Marekani ni muungaji mkono wakuu wa ugaidi katika eneo

Amesema vita vya Syria viliibuliwa ili kuleta mabadiliko makubwa Mashariki ya Kati na hivyo Hizbullah itaendelea kushiriki katika vita hivyo hadi  mwisho. Kuhusiana na hujuma haramu ya Saudia dhidi ya taifa la Yemen, Sayyed Nasrallah amesema hujuma hiyo imeathiri vibaya maisha ya watu zaidi ya milioni 20.

Aidha amelaani mashirika ya kimataifa kwa kushindwa kuchukua hatua za maana kumaliza ukatili wa Saudia dhidi ya raia wa Yemen.

3461288

captcha