IQNA

Uturuki yalaaniwa kwa kufunga Televisheni za Waislamu wa Kishia

12:05 - January 25, 2017
Habari ID: 3470811
IQNA-Serikali ya Uturuki imelaaniwa vikali kwa kuamuru kufungwa televisheni mbili za Waislamu wa madhehebu ya Shia ambazo zilidaiwa kueneza "propaganda dhidi ya serikali".

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, ON4TV na Kanal12 zilifungwa kwa mujibu wa sheria ya kupambana na ugaidi.

Stesheni hizo zimefungwa huku kukiwa na wasiwasi kuhusu wimbi la ukandamizaji vyombo huru vya habari nchini Uturuki.

Wakati huo huo, Sheikh Salahuddin Ozgunduz, kiongozi wa Jumuiya ya Jaafari nchini Uturuki amekosoa amri ya serikali ya kufungwa kanali hizo mbili na kusema kuwa hatua hiyo imesababishwa na chuki kipofu za kimadhehebu. Ameongeza kuwa hatua hiyo ya serikali inakinzana na sheria za Uturuki na kwamba kanali hizo za televisheni hazijawahi kuwa na mahusiano yoyote na vitendo vya kigaidi.

Ameendelea kusisitiza kuwa, kanali hizo zinazotangaza mafundisho ya Ahlu Bayti wa Mtume (saw) hazijawahi kuhusika na uchochezi wa kigaidi na kwamba, ikiwa serikali ya Ankara imeamua kuzifunga kwa sababu tu ya chuki za kimadhehebu, basi ni suala la kusikitisha sana.

Sheikh Salahuddin Ozgunduz, amesema kuwa wakati kanali za televisheniza Waislamu wa Shia zikifungwa, kuna kanali ambazo zimekuwa zikifanya kazi ya kuchochea fitina usiku na mchana sambamba na kuwasahaulisha raia wa taifa hilotamaduni bora za Kituruki.

Jaribio la mapunduzi ya kijeshi lililofeli nchini Uturuki mwezi Julai mwaka jana limesababisha maelfu ya wafanyakazi wa serikali kufutwa kazi huku wengine wakikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na mapinduzi hayo.

Aidha idadi kubwa ya vyombo vya habari vimepokonywa vibali na kufungwa huku waandishi habari wengi wakikamatwa na kukandamizwa.

http://iqna.ir/en/news/3462023

captcha