IQNA

Bango la kutaka Waislamu wafukuzwe Marekani katika ukuta wa chuo kikuu

12:58 - February 15, 2017
Habari ID: 3470850
IQNA: Waislamu nchini Marekani wameingiwa na hofu Zaidi baada ya mabango yenye maandishi ya "Marekani isiyo na Waislamu'' kupatikana Jumatatu katika Chuo Kikuu cha Rutgers mjini New Jersey siku ya Jumatatu.

Bango hilo limepatikana katika ukuta wa jengo ambalo wanafunzi Waislamu wanalitumia kila siku kwa ajili ya sala na shughuli zao zingine.

Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani (CAIR) tawi la New Jersey limetoa taarifa likilaani chuki hiyo dhidi ya Waislamu. "Bango hilo limeonyesha chuki na wito usio wa moja kwa moja wa kuwaangamiza kwa umati Waislamu. Haipaswi kustahamili hisia kama hizi," amesema James Sues mkurugenzi wa CAIR New Jersey.

Ameongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona chuki dhidi ya Uislamu zikiwa zimeongezeka katika miezi ya hivi karibuni hasa baada ya kuchaguliwa Donald Trump kuwa rais wa nchi hiyo.

Wakati huo huo CAIR imewataka Waislamu na taasisi za Kiislamu Marekani kuchukua hatua za tahadhari kutokana na ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu.

3462219

captcha