IQNA

Kongamano la Kimataifa la Hija lafanyika Makka

15:11 - August 26, 2017
Habari ID: 3471143
TEHRAN (IQNA)-Kongamano la Kimataifa la Hija linafanyika Agosti 26-27 katika mji takatifu wa Makka ambapo wanazuoni wa Kiislamu kutoka mabara yote duniani wanashiriki.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi Arabia na anwani yake ni "Hija; Jukwaa la Amani".

Washiriki katika kongamano hilo wanajadili maduhui kama vile, "Uislamu, Dini ya Amani", "Utajiri wa Kifiqhi wa Ibada ya Hija na Taathira zake katika Kufikia Amani," "Maadili ya Amani katika Ibada ya Hija", na "Amani katika Hija kwa Wanadamu, Wanyama, Mimea na Mazingira."

Aidha waandalizi wanasema mada zingine ambazo zinajadiliwa katika kongamano hilo ni "Mafunzo ya Mtume SAW katika Hotuba ya Hajjatul Wida (Hija ya Mwisho) na namna ya kufikia amani katika familia na jamii," na "Utumizi wa Mfumo wa Habari wa Kidijitali na taathira zake katika kuwahudumia Mahujaji."

Mahujaji zaidi ya milioni mbili wanatazamiwa kutekeleza Ibada ya Hija mwaka huu.

3633813

captcha