Kwa mujibu wa taarifa, msikito huo umebuni bakodi ambayo inawawezesha wanaofika hapo kuswali kuichukua taswira yake kwa kutumia simu za mkononi na hapo wanaweza kupata nakala ya Qur'ani.
Nakala hiyo ya Qur'ani ya kidijitali ina lugha mbali mbali na pia ina qiraa kwa sauti za wasomaji mashuhuri duniani.
Hatua hii imechukuliwa baada ya wataalamu wa afya kushauri kuwa waumini kwa sasa wasitumie misahafu iliyo misikitini kutokana na hofu ya kuambukizana ugonjwa wa COVID-19. Misikiti inawashauri waumini wasome Qur'ani kwa kutumia vifaa binafsi vya kielektroniki kama vile simu za mkononi au tableti.