Rais wa Syria aliyasema hayo siku ya Jumatano katika hotuba aliyotoa kwenye kikao cha ufunguzi wa bunge la nchi hiyo. Bashar al Assad amekosoa sera za Marekani, Uturuki na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya nchi yake na kuitaja sheria ya Marekani ya Caesar kuwa ni "Uharamia wa Baharini".
Rais wa Syria, Marekani ina utegemezi kwa makundi ya kigaidi katika siasa zake za nje, kiasi kwamba inaliunga mkono hata kundi la ISIS au Daesh ambalo inalitaja kama kundi la magaidi wabaya.
Rais wa Syria ameitaja sheria ya Caesar kama awamu mpya ya utoaji mashinikizo makali zaidi dhidi ya nchi yake na akasema, vikwazo hivyo havitenganiki na hatua zingine za Marekani dhidi ya Syria, na kwamba kila pale Washington inapokuwa imeshindwa kufikia malengo yake huwa inatumia silaha ya vikwazo. Assad ameufananisha utumizi wa vikwazo unaofanywa na Marekani na mbinu iliyokuwa ikitumiwa hapo zamani na maharamia wa baharini.