IQNA

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Chelsea FC kuandaa dhifa kubwa ya futari mwezi wa Ramadhani

22:15 - March 14, 2023
Habari ID: 3476705
TEHRAN (IQNA) – Klabu ya Soka ya Chelsea ya Ligu Kuu ya Uingereza (EPL) imetangaza kuwa uwanja wake, Stamford Bridge, utakuwa mwenyeji dhifa yake ya kwanza ya wazi ya Futari katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

 Jumapili Machi 26, Wakfu wa Chelsea utakuwa wenyeji wa ‘Futari ya Wazi’ pembeni mwa uwanja wa mpira kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, ambayo itakuwa ya kwanza kwa klabu hiyo na pia itakuwa futari ya kwanza ndani ya uwanja wa EPL.

Tukio hili kubwa zaidi la la kijamii nchini Uingereza katika Mwezi wa Ramadhani, litakuwa fursa kwa Waislamu wanaotazama Ramadhani wakati muafaka kukusanyika ili kufuturu pamoja na kutoa nafasi kwa mazungumzo na ushirikiano.

Idadi kadhaa ya misikiti na wanachama wa jumuiya ya Kiislamu ya eneo la Chelsea kama vile mashabiki na wanafunzi wa shule wataalikwa kuhudhuria dhifa hiyo, pamoja na wafanyakazi wa Chelsea FC.

Dhifa hiyo ya futari iliyopewa jina la ‘Open Iftar’ itaendeshwa kwa ushirikiano na Mradi wa Ramadan Tent Project (Hema la Ramadhani), shirika la usaidizi lililoshinda tuzo lililoanzishwa mwaka wa 2013 kwa dhamira ya kuleta jamii pamoja na kukuza uelewa wa Ramadhani.

Ramadan Tent Project, ambao mwaka huu wanasherehekea kumbukumbu ya miaka 10, huandaa Tamasha la kila mwaka la Ramadhani ambalo ni sherehe ya kila mwaka ya sanaa, utamaduni na ubunifu inayohamasishwa na mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Omar Salha, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Hema la Ramadhani, alisema: 'Kwa muongo mmoja uliopita Mradi wa Hema la Ramadhani umeunganisha na kuwakutanisha zaidi ya watu nusu milioni kutoka kila aina kupitia Tamasha lake la kila mwaka la Ramadhani na mpango mkuu wa Open Iftar.

‘Tuna heshima ya kuleta Open Iftar Stamford Bridge, katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 na mada yetu ya 2023 ya “Belonging”, na kufanya kazi kwa ushirikiano na Klabu ya Chelsea.

Simon Taylor, mkuu wa Chelsea Foundation, alisema: ‘Nina furaha kutangaza Iftar yetu ya Wazi pamoja na Mradi wa Hema la Ramadhani na tunajivunia kuwa klabu ya kwanza ya Ligi Kuu kufanya hivyo. Kuitambua Ramadhani na jumuiya yetu ya Kiislamu ni kipengele muhimu cha kazi yetu katika kukuza uvumilivu wa kidini na ninatazamia kuwakaribisha watu wote Jumapili tarehe 26 Machi.’

3482804

Kishikizo: chelsea futari uingereza
captcha