Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,Sadio Mane ameonekana akisoma Qur’ani Tukufu ndani ya ndege kabla ya mechi dhidi ya Bayer Leverkusen na kuvuia hisia chanya miongoni mwa Waislamu kwenye mitandao ya kijamii.
Thomas Müller, mchezaji wa Ujerumani wa Bayern Munich, alichapisha picha yake akiwa na Sadio Mane, mchezaji mwenzake Muislamu akiwa anasoma Qur'ani Tukufu wakiwa ndani ya ndege.
Sadio Mane ni maarufu sana mingoni mwa Waislamu duniani kwa sababu ya kujitolea kwake katika kufungamana na mafundisho ya Uislamu.
Katika mahojiano na Daily Mail, mchezaji huyu wa Senegal alisisitiza kuwa hajawahi kugusa pombe katika maisha yake yote.