IQNA

Waislamu Australia

Jiji la Australia laidhinisha ujenzi wa msikiti wa kwanza kufuatia ongezeko la Waislamu

18:59 - June 09, 2023
Habari ID: 3477124
Baraza la Jiji la Wagga Wagga katika eneo l New South Wales Riverina nchini Australia limetoa idhini kwa jamii ya Waislamu kujenga msikiti wao wa kwanza ambao utajumuisha ukumbi wa maombi wenye uwezo wa kuchukua watu 100.

 Mmoja kati ya viongozi wa Waislamu eneo hilo, Shamsul Haque amesema Waislamu wana furaha kwa kupata kibali cha ujenzi kwani wamekuwa wakichangisha fedha kwa ajili ya mradi huo tangu 2009.
"Tulipokuja hapa kutoka Bangladesh, jambo la kwanza tulilogundua ni kwamba hakukuwa na msikiti  Wagga au miji inayozunguka," Dk Haque alisema.
"Tumekuwa tukiswali kila wiki katika sehemu mbalimbali na tulihitaji mahali pa kudumu ambapo tunaweza kusali."
Idadi ya Waislamu wa Wagga Wagga imeongezeka kutoka watu 92 hadi zaidi ya 650 katika miongo miwili iliyopita, kulingana na data ya sensa.
Dk Haque na mkewe, Jesmin Aktar, walisema msikiti huo utatumika kama kitovu cha jamii na kuvutia Waislamu zaidi katika eneo hilo.
"Sio tu mahali pa Sala. Watu wanaweza kuja pamoja ili kubadilishana uzoefu wao na kufahamian," Dk Aktar alisema.
Mradi huo wa msikiti ulizinduliwa na Jumuiya ya Waislamu wa Riverina Wagga Australia (MARWA).
Kundi hilo limekusanya zaidi ya dola milioni 1.8 kupitia michango kutoka kote Australia na ng'ambo. Msikiti huo utagharimu takriban dola milioni 2 kuujenga na MARWA inatumai kuwa utakamilika katikati ya 2024.

3483870

captcha