IQNA

Wafanyaziyara wa Arubaini waliandika aya za Qur'ani Tukufu ili Kujibu udhalilishaji

10:07 - September 12, 2023
Habari ID: 3477586
KARBALA (IQNA) – Katika kampeni ya kuheshimu Qur’ani Tukufu, makumi ya wafanyaziyara wa Arubaini waliandika aya za kitabu hicho kitukufu wiki iliyopita.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa na kituo chenye mfungamano na Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS), ilikaribishwa kwa moyo mkunjufu na makumi ya wanazuoni, wahubiri, na wafanyaziyara kutoka nchi mbalimbali walioshiriki katika matembezi ya Arubaini wiki iliyopita.

Montazer al-Mansouri, afisa wa Ofisi ya  Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS), alisema mpango huo ulizinduliwa chini ya jina la "Kujitolea kwa Qur'ani Tukufu kama jibu kwa vitendo vya kudharau Qur'ani katika nchi chache za Magharibi.  

Aliisifu Qur’ani Tukufu iliyoandikwa kwa mkono kama toleo  refu zaidi la maandishi matukufu ambayo yameandikwa kwenye kitambaa cha urefu wa mita 300.  

Programu mbalimbali zilifanyika mwaka huu kwa ajili ya kuheshimu Qur'ani Tukufu wakati wa matembezi ya Arubaini ambayo yalivutia zaidi ya watu milioni 20 kutoka nchi mbalimbali kwenda Iraq.

Arubaini ya mwaka huu inakuja huku kukiwa na wimbi jipya la vitendo vya uvunjifu wa heshima wa Qur'ani Tukufu ambavyo vinaruhusiwa kutokea katika mataifa ya Nordic, hasa nchini Sweden na Denmark, chini ya kivuli cha uhuru wa kujieleza.  

Mipango na kampeni nyingi zimefanyika mwaka huu kuheshimu Qur’ani Tukufu wakati wa matembezi ya Arubaini na mamilioni ya wafanyaziyara wanaofanya safari hiyo ya kilomita kwa miguu.  

Tafsiri ya Aya Kubwa za Qur'ani  Tukufu Ziling'aa huko Bain-ul-Haramain

Maombolezo ya Arubaini ilisimama kama kutaniko la ajabu na kubwa la kidini katika kiwango cha kimataifa, na zaidi ya wafanyaziyara milioni 20 walihudhuria, Tukio hili kubwa linaashiria siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW).

 

3485120

 

captcha