IQNA

Waislamu wa Kenya Wataka Balozi wa Utawala wa Israel Afukuzwe katika Nchi

9:54 - October 17, 2023
Habari ID: 3477745
NAIROBI (IQNA) - Waislamu wa Kenya wameitaka serikali ya nchi hiyo ya Kiafrika kuvunja uhusiano na utawala wa Israel kutokana na mauaji yake ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.

Viongozi hao wa kisiasa na kidini wa Kiislamu pia walizindua mfululizo wa shughuli wanazopanga kuzifanya ili kuonyesha uungaji mkono wao kwa Wapalestina waliozingirwa.

Waliitaka serikali ya Nairobi kumfukuza balozi wa Israel na kumuita tena mjumbe wa Kenya katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Wabunge Omar Mwinyi na Yusuf Hassan, seneta wa zamani Billow Kerrow na mwenyekiti wa Jukwaa la Viongozi wa Kiislamu(Namlef) Sheikh Abdullahi Abdi walikuwa miongoni mwa viongozi wengi waliotoa wito huo.

Pia wameitaka jumuiya ya kimataifa kuwasaidia Wapalestina waliokwama huko Gaza na kunyimwa huduma za kimsingi.

Nchi Zaidi Zinajiunga na  Wapalestina Kulaani Unyama wa Israel huko Gaza

Tunatoa wito kwa serikali ya Kenya kukata uhusiano na Israel mara moja, Msimamo uliochukuliwa na Umoja wa Afrika ni kuunga mkono Palestina huru, Kenya lazima ifuate msimamo huu kwa sababu ya kuwa mwanachama wa AU, Sheikh Abdi aliwaambia waandishi wa habari wakati wa mkutano na wanahabari katika Msikiti wa Jamia jijini Nairobi Jumapili.

Naye Mwinyi, alisema atatoa hoja Bungeni kujadili kinachoendelea Palestina.

Aidha amezitaka serikali zote halali duniani kujitenga na utawala wa Kizayuni unaoungwa mkono na Marekani katika kutekeleza jinai dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina.

Kila mtu anapaswa kusema na kulaani Israel kwa sababu kukaa kimya ni kuunga mkono uonevu, aliongeza kwa kusema tunaiunga mkono Palestina.

 


3485602

 

 

captcha